Dokii Aeleza Mengi Kuhusu Rich Mavoko na Mahusiano yake


Muigizaji na mtangazaji Dokii Wanceslaus ambaye ni ndugu wa msanii Rich Mavoko, ameibuka na majibu kuhusu kuwa na Mwanaume mzee kwenye mahusiano yake.


Akiieleza EATV & EA Radio Digital Dokii Wanceslaus amefunguka

"Sasa Mimi Mwanaume mzee wa nini si nitamuumiza tu, kwanza nitampa kibarua ambacho hawezi kufanya, tunaweza kupata hata kesi nyingine nikajikuta nipo jela. nitampelekesha mzee miondoko ambayo hajazoea kwa mfano mzee amezoea miziki ya 'blues' halafu unampelekea kisingeli nitakuja kuambiwa Dokii nimeuwa", amesema.

Ameendelea kusema bado hajafikia miaka ya kuwa na mahusiano na wazee kwa  sababu ni dada wa makamo na atatafuta mtu wa "size" yake pia hatarajii kuwa na mzee wala watoto kwenye mapenzi.

Aidha amesema kila mtu ana chaguo lake katika mahusiano ila anachokiangalia ni utofauti na akichagua mwanaume huwa  anamuangalia kama anaendana naye au haendani naye.

Pia anapendelea mwanaume ambaye hajaoa na aliye 'single' hata akimuhitaji apate muda wa kumfurahisha na awe anajua kucheza miziki ya kikubwa.

Aidha Dokii amesema Rich Mavoko ana maisha yake mazuri tu nje ya mitandao ikiwemo kuwa baab wa mtoto mmoja na anawajibika vizuri kumtunza mwanaye.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad