Ebitoke Asimulia Alivyoanza Mapenzi Na Mlela



MIONGONI mwa stori zenye wafuatiliaji wengi kuhusu mastaa wa Bongo ni ‘couple’ mpya jijini inayowahusisha waigizaji Ebitoke na Yusuph Mlela ambao wameendelea kuvitengeneza vichwa vya habari tangu walipoamua kuyaweka hadharani mahusiano yao.



Ebitoke amefika kwenye studio za +255 Global Radio leo Septemba, 20 2018 na kupiga stori na watangazaji wa kipindi cha Mid Morning Fresh ambapo amefungukia mambo mengi ikiwemo mwanzo wa safari yake ya uigizaji, changamoto, mahusiano na mengine mengi.



Wema na Lulu ni miongoni mwa wasichana waliokuwa wakimvutia mrembo Ebitoke ambaye kwa namna moja amefanikiwa kujitengenezea nafasi nzuri ya ushawishi kwenye jamii. Ebitoke ambaye ana asili ya mkoani Kagera amesema alilazimika kuondoka nyumbani kwa mjomba wake na kuingia mtaani alipoanza kuhangaikia ndoto zake kwa kufanya kazi za ndani na usaidizi wa mama-lishe.

“Nilikuwa napenda sana nije kuwa mwigizaji wa Bongo Muvi lakini mjomba wangu hakupenda,  hivyo nililazimika kuondoka nyumbani kwa kutoroka na kuingia mtaani ambako nilikutana na maisha magumu sana.  Nimefanya kazi za ndani, mama-lishe na kuna muda nilikata tamaa kabisa,”  amesema Ebitoke.

Ebitoke amefungukia pia ishu ya kutoka na Ben Pol ambapo amedai kuwa alijisikia kuweka hisia zake mtandaoni baada ya kumkosa Ben Pol na kumwambia alivyokuwa anajisikia juu yake.

“Nilimpenda kweli Ben na zile zilikuwa hisia zangu,  ni vile tu yeye hakuwa serious,” amesema.

Ebitoke alitumia hiyo kama nafasi ya kuelezea mapenzi yake na Yusuph Mlela ambaye walikutana Zanzibar na mapenzi yao kuanzia huko.


“Yusuph ameoniongezea thamani kwani tofauti na mapenzi, sisi tunafanya kazi kweli, tulikutana Zanzibar tukawa karibu then tukajikuta vitu vimeungana, kazi yetu mpya ni maisha halisi tangu siku tulipokutana,” alisema Ebitoke.

Kuhusu kuondoka Timamu Comedy, Ebitoke amesema ni changamoto za kikazi zilitokea akaamua kuachana na uongozi huo lakini amesema yeye na Timo ni washikaji na wamekuwa wakichati na kupongezana kwa kila hatua wanayopitia.

“Timo amenifundisha kutokuwa na tamaa, kukata tamaa, niwe na nidhamu na juhudi pia, amenijenga sana sitachoka kumuongelea vizuri,” amesema.

Mwisho Ebitoke amefungukia ishu ya kukata tamaa ambapo alisema amekuwa akijiwazia mazuri zaidi na kumtanguliza Mungu kuliko vingine, hivyo suala la kukata tamaa kwake ni ndoto.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad