Familia ya Robert Mugabe yakasirishwa na mipango ya mazishi Zimbabwe 'inayokwenda kinyume na wosia wake'
1
September 12, 2019
Familia ya Robert Mugabe inasema imeshutushwa kwa kutoshauriwa na serikali kuhusu mipango ya mazishi ya aliyekuwa rais wa Zimbabwe.
Mugabe, alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 95, wakati akiwa anapokea matibabu katika hospitali moja huko Singapore.
Mwili wake unatayarishwa kulazwa ili kupewa heshima za mwisho kitaifa katika uwanja wa soka katika mji mkuu wa Zimbabawe, Harare.
Familia yake na serikali zinatofuatiana kuhusu sehemu atakapozikwa Mugabe.
Familia yake inasema mwili wake utalazwa kuonekana mara ya mwisho nyumbani kwake katika kijiji cha Kutama Jumapili usiku, na atazikwa katika mazishi ya faragha.
"Mwili wake utapewa heshima za mwisho Kutama Jumapili usiku na kufuatwa na mazishi ya faragha - pengine Jumatatu au Jumanne - na sio katika makaburila ya kitaifa ya mashujaa wa uhuru. Huo ni uamuzi wa familia nzima," binamu yake, Leo Mugabe ameliambia shirika la habari la AFP.
Rais Emmerson Mnangagwa alimtangaza Mugabe kuwa shujaa wa kitaifa baada ya kifo chake, na kuashiria kuwa anapaswa kuzikwa katika eneo hilo la kitaifa.
Waziri wa elimu Paul Mavhima amesema hakuna shaka Mugabe anasathili kuzikwa kama shujaa wa kitaifa.
"Mtu muhimu wa aina hiyo, ambaye mazishi yake yatahudhuriwa na zaidi ya viongozi 50 wa taifa na wa zamani. Muasisi wa taifa hili hakupaswi kuwa na majadiliano ya hilo. hakupaswi kuwa na mzozo wowowte. Uamuzi unapaswa kuwa wa wazi, anastahili kuzikwa katika kaburi la kitaifa,"ameiambia BBC.
"Itakuwa ni makosa makubwa kuwa na mpiganiaji uhuru wa taifa hili, mhamasishaji mkubwa wa raia wa Zimbabwe kuzikwa katika eneo jingine lolote kando na kaburi la itaifa. Wito ni kuiomba familia - huyu sio wenu tena, ni kiongozi wa taifa. Ni kiongozi wa Afrika. Ni kiongozi duniani, Anastahili kupewa heshima anayoistahili . Kwahivyo atazikwa katika kaburi la kitaifa''
Tags
Yes.!!! He was and is a National icon.
ReplyDeleteA rear Freedom fighter .
A symbol of Zimbabwe Historythat will never fed and you cannot mention Zimbabwe without Robert Mugabe being part of the heroic Story.
Lalaa mahali pema Shujaa wetu.