Gwajima awataka Kinana na Mzee Makamba kumuangukia JPM


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema Rais Magufuli amevunja rekodi ya Afrika nzima kwa kuwasamehe akina Nape, January Makamba na Ngeleja,

Akizungumza katika ibada ya jumapili jana Sptemba 15 Jijini Dar es Salaam amesema, kwa Marais wote wa Kiafrika na duniani kote, ni ngumu sana kuwasamehe maadui hasa unawaoona wanakusema vibaya, na ni watu wako wa karibu.

Amesema, Rais Magufuli alivunja rekodi ya Marais wa Kiafrika, pale ambapo aliwasamehe Nape, Makamba na Ngeleja ingawa alisema inaumiza.

Amesema, anawaomba Abdulrahman Kinana na Mzee Makamba wajipe moyo mkuu wakaombe msamaha sababu wenzao wameshaomba msamaha na kitendo cha wao kukaa hivo hivo kitawaumiza.

“Mimi nawatia moyo na wao, angalau wajikongoje  angalau ndani ya wiki mbili zijazo wakaombe msamaha,” Alisema Gwajima.

Aidha amewataka waumini kumpongeza Rais Magufuli kwa kuonyesha Moyo mzuri wa kusamehe,

Askofu Gwajima pia ameipongeza hatua ya Rais Magufuli ya kubadilisha uongozi kwenye idara ya usalama wa Taifa kwani kufanya kwake huko kunaashiria  kulikua na mambo ya ajabu yaliyokuwa yakiendelea nchini ambayo yanaweza kubadilika na kuondoka kabisa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad