Haji Manara Ashindwa Kuvumilia Ampa za Uso Mkuu wa Mkoa wa Kagera "Tutashangilia Alafu uje Utuweke lock-up kwa Cheo Chako"

Alichokiandika Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, kuhusiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti juu ya kauli yake ya kuwataka Wanakagera waishangilie Kagera Sugar pekee. "Kama kweli RC huyu mwenye cheo kikubwa kijeshi kasema haya, basi tuna kazi kubwa sana katika ustawi wa mpira wetu.
.
"Utaweza kuifunga midomo ya Wanasimba kwa plasta au gundi gani?

Kitu pekee kitakachowanyima fursa ya kuishangilia leo Simba uwanjani ni bunduki tu.

Tutashangilia na Insha'Allah tutawafunga halafu uje utuweke lock-up kwa cheo chako!! Sijui baadhi ya viongozi wetu wanakwama wapi?

Yaani utuzuie kushangilia timu yetu ndani ya nchi yetu?

Haya tunaita madaraka ya kulevya ambayo Rais wa nchi hii hayataki!!."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad