Nyota wa Bongo Fleva Rajab Kahali ‘Harmonize’ amesema yuko mbioni kuzindua albamu yake mpya mwishoni mwa mwaka huu itayojulikana kwa jina la Bongo To Lagos ambayo itajumuisha wasanii wa Afrika Mashariki na Afrika Magharibi.
Harmonize amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa BBC, Salim Kikeke baada ya kumaliza kufanya shoo yake nchini England.
“Itakuwa ni collaboration zaidi, ni kama vile East meets West. Lengo ni kuwaonesha wasanii wa Afrika Magharibi watambue zaidi mziki wetu, waijue Bongo Fleva kiundani. Mimi naita Afro East kwa sababu mziki wa Afrika unatambulika kama Afro West, sasa kwa sababu wa kwetu una Kiswahili ndani tunaita Afro East.”
Alipoulizwa kwanini wasanii wasitumie muziki wa Kitanzania kutangaza sanaa yao badala ya kutumia muziki wenye mahadhi ya Kinigeria, Harmonize amejibu: “Muziki ni kama burger, juu unaweka mkate, chini mkate na katikati utachagua uweke kuku au nyama lakini ni burger tu. Kwa hiyo muziki ni ule ule ila ni kuchanganya tu ladha kwa pamoja.
Ameongeza pia atakuwa na mazungumzo na wasanii wenzake wa Afrika Mashariki kujadili namna ya kuupeleka muziki wao mbele kama wenzao wa Afrika Magharibi.
Amesema uwepo wa watu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki nchini England anaamini ni sapoti tosha ya wao kuweza kuupenyeza muziki wao nchini humo kirahisi.
Vile vile Harmonize amesema mapema mwaka 2020 ana mpango wa kuandaa shoo ambayo itafanyika Ukumbi wa O2 Arena, ambao ukumbi mkubwa zaidi uliopo jijini London nchini England.
Hata hivyo, amekataa kuzungumzia tetesi zinazozagaa kuwa ana mpango wa kujitoa katika lebo ya WCB, ambayo ipo chini ya Diamond Platnumz.
Maoni ya watu mbalimbali;
skytanzania
Awesome 4 minutes!
shaks0217
Hivi bro si unafanya bbc swahili huyo mmakonde kinge cha nini sasa????you know you know in Magufuli voice
namkwahe_
Raia acheni kuchonga kwa mwana. Kapiga interview poa sana. Kuweni waelewa, hii interview haitazamwi na Swahili-speaking countries pekee. Amefanya jambo jema kuchanganya lugha ili fans wake around the world waelewe anachozungumza japo kwa ufupi.
issajohn840
Apige Kazi ushndan umerud kweke alikiba tupa kule
newtonlamec
mmmmmmmmmmmm mmkonde kaenda juzi uk ety kasahau kiswahili wakati kikeke anamwiaka huko hajasahau kiswahili tubadilike jaman tujivunie lugha yetu
tita_noboa
sasa anaongea kiingereza kaulizwa kwa kiingereza
lilystopper
MMAKONDE MMAKONDE TUUU HAFADHILIKI 😂
top_lifesolutions
Huo ni utoto unahojiwa kwa kiswahili unajibu kwa kingereza hiyo BBC swahili hapo ingehojiwa kingereza ungeanza kukata kucha acha utoto
2406_lee
Kaulizwa kisw anajibu kingeereza🤣🤣🤣 mswahili🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽
kapusidaniel
Ameuliza kiswahili anachangaya na kiingereza feki . Aibu tuuu
oficialaalikiba
Bro ako anakuongolesha kiswahili sio kama hajui ngeli 😂 jua muktadha sio you know wat wat
georgeminja82
Wadau mi cjaelewa..huyu jmaa katoka wcb ila mbona bdo cheni yao anayo au inakuwaje!..au kuna kamchezo hawa sanatufanyia