Hili ni Funzo Kubwa Katika Mapenzi, Tujaribu Kuchukua Hatua ya Busara na ya Kiutuzima..



Zilipita sekunde, dakika, masaa, siku, miezi na hatimaye miaka sasa tangu niachane na mwanamke niiyependana naye sana. Baada yake nimekuwa na mahusiano mengine kadhaa ambayo hayakuwa na msingi wa upendo, yalikuwa ilimradi mahusiano tu.

Chanzo kubwa cha mahusiano yangu kuvunjika na kipenzi changu ni tatizo letu wanaume wengi kwa sasa, nilipendana naye kipindi nipo chuo, sikuwa na stable economy kabisa.. akapata vishawishi na hapo tumeshakaa pamoja miaka kama mi tatu (Though silaumu kwa kuwa ameenda kwa mwingine kwa sababu hata sisi wanaume tungejaribu kuvaa viatu vyao tukawa wanawake tusingeweza vumilia wanaume wasio na pesa).

Nimekaa na kutafakari ila nimeona bado moyo wangu uko kwake, hata kama kawa na wanaume wangapi still i love her, ninachofanya ni ishu moja, nipo najipanga kiuchumi niwe na flow kubwa ya Pesa, kisha nimchukue au nimyanganye kwa mshikaji aloko naye sasa.

Wanaume wenzangu tukiwa hatuna Pesa sio kwamba hatupendwi.. tunapendwa sana tu ila tatizo ni mwanamke anakosa security ya future yake kwako, anaweza kuwa na wewe kwa sababu ya upendo ila uvumilivu wao unawafikaga mwisho, Tafadhali tusiwalaumu hawa viumbe wanapotuacha kisa hatuna pesa.. wamevumilia mpaka wakafika mwisho.

Nadhani kila mtu ni shahidi wa kupendwa hata wakati ule hana kitu, je hata kama huyo mwanamke alikuacha siku ukipata kitu huoni kwamba ni chaguo sahihi?

Mapenzi ya dhati ili yadumu pesa kidogo inabidi iwepo!

Pesa ni muhimu ila Upendo wa dhati muhimu zaidi

Binafsi nitamrudisha wa kwangu,,soon nitaleta mrejesho tuombeane tu SHIMO LITEME!
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad