Historia ya Vita vya Kagera Tanzania na Uganda Kwa Ufupi
0
September 20, 2019
Vita kati ya Tanzania na Uganda, au Vita ya Kagera ilidumu kwa miezi sita kuanzia Novemba 1978 hadi Aprili 1979 na ndiyo iliyouangusha utawala wa Iddi Amin Dada uliodumu kwa muda wa miaka minane
Idd Amin aliingia madarakani Januari 25, 1971 alipoiangusha Serikali ya Dkt. Milton Obote na aliondoka Aprili 11, 1979 wakati majeshi ya Tanzania na ya Uganda yaliposhirikiana kumuondoa
Mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Uganda ulianza Januari 25, 1971 baada ya Idd Amin kuipindua Serikali ya Obote na Rais wa Tanzania wa kipindi hicho alimpa Obote hifadhi ya kisiasa
-
Mambo mengi ambayo yangeweza kusababisha Vita ya Kagera yalikuwa yametendeka tangu Januari 1971 hadi Oktoba 1978, lakini kwa kipindi chote hicho hakuna vita iliyozuka
Vita hiyo ilianza rasmi siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Uganda, Oktoba 9, 1978 baada ya mwanajeshi wa Uganda kuvuka mpaka na kuingia Tanzania kukutana na mpenzi wake ambaye alikuwa raia wa Tanzania
#JFHistoria
Tags