Jaji Mkuu Aomba DNA Itumike Katika Uchunguzi Kesi za Ubakaji

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema kuwa ufanyike mkakati wa kuangalia matumizi ya kuchukua sampuli kwa ajili ya kipimo cha vinasaba (DNA) ili visaidie kurahisisha upatikanaji wa ushahidi kwa watuhumiwa wanaofanya vitendo vya ubakaji na kulawiti watoto hapa nchini.

Ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kutembelea mahakama na kukagua miradi mipya ya ujenzi wa majengo ya mahakama mkoani Njombe ambapo amesema bado hajaona matumizi ipasavyo ya kipimo cha vinasaba (DNA) na kwamba anazani ipo haja matumizi ya kuchukua sampuli ya vinasaba ikatumika kupata ushahidi wa kesi za ubakaji na kulawiti.

Aidha, Jaji Mkuu wa Tanzania akizungumzia lengo la ziara katika mkoa wa Njombe amesema kuna jopo la majaji wanne waliofika kufanya kikao cha kesi za rufani akiwemo yeye mwenyewe ili kuzitolea majibu.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendaka amemweleza Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma alipokuwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo kuwa hadi sasa jumla ya washitakiwa wa matukio ya mauaji mkoani hapo wapo zaidi ya 156 na kwamba upo umuhimu wa kuwa na Mahakama Kuu mkoani Njombe
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad