Jeshi la Iran lasema liko tayari kwa hali yoyote


Jeshi la wanamapinduzi wa Iran limeonya kuwa litashambulia kundi lolote litakaloleta uchokozi dhidi ya nchi hiyo.

Taharuki katika eneo hilo la ghuba imeongezeka baada ya mashambulizi dhidi ya viwanda vya mafuta nchini Saudi Arabia mwishoni mwa wiki iliyopita na Marekani na Saudia Arabia zimeilaumu Iran kwa mashambulizi hayo.Iran imekanusha kuhusika.

Katika mkutano na wanahabari ulioonyeshwa kupitia kituo cha habari cha runinga nchini humo, mkuu wa jeshi hilo meja jenerali Hossein Salami ameonya kuwa kiwango chochote cha uchokozi hakitavumiliwa na kwamba wanakadiria adhabu na wataendelea hadi kuharibiwa kabisa kwa kundi lolote la uchokozi.

Salami amesema kuwa Iran haitaki kuanzisha vita lakini akasisistiza kuwa vikosi vyake vimefanya mazoezi ya vita na viko tayari kwa hali yoyote ile.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad