Jeshi la Polisi Latumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Wanafunzi Chuo cha Ualimu Moshi


Jeshi la Polisi limezuia maandamano ya wanafunzi zaidi ya 400 wa Chuo cha Ualimu Moshi kilichopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, kisha kuwakamata baadhi yao baada ya kufunga barabara wakishinikiza serikali kuingilia kati sakata la utapeli wa zaidi ya milioni 75 za malipo ya ada.


Shinikizo hilo linachukuliwa na Wanafunzi hao baada kuzuiliwa kuingia kwenye chumba cha mtihani kutokana na Malipo yao ya Ada waliyolipa kupitia Benki  kutoonekana kwenye account  ya chuo hicho


Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo la nchi hii watoto wa masikini hawathaminiwi kabisa hata wasiposoma kuna baadhi ya watu wanaona sawa tu, hao wanafunzi ilitakiwa wasikilizwe madai yao si kupigwa mabomu ya machozi, madai yao ni ya msingi kwa sababu wamelipa ada lakini malipo yao hayaonekani kwenye akaunti ya chuo hicho kwa maana hizo hela zimechukuliwa na watu ambao hawana hata hofu ya Mungu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad