Jinsi Bilionea Aliyeuawa Kenya Alivyozikwa...Miradhi Yasomwa


Nairobi, Kenya. Mwili wa mfanyabiashara maarufu nchini Kenya aliyeuawa kisha kutupwa katika tangi la maji nyumbani kwake umezikwa.

Tob Cohen ambaye ni bilionea mwenye asili ya Uholanzi aliyekuwa akiishi nchini humo amezikwa jana Jumanne Septemba 24 kwa mila za Kiyahudi jijini Nairobi.

Mke wa mfanyabiashara huyo, Sarah Wairimu ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauji ya mumewe aliwasili katika makaburi ya Kiyahudi yaliyopo katika barabara ya Wangari Maathai saa 9.00 alasiri.

Sarah alihudhuria mazishi hayo baada ya mahakama kumruhusu mjane kushiriki shughuli hizo baada ya kuwasilisha ombi lake Mahakamani.

Katika maamuzi hayo, Mahakama iliagiza afisa wa gereza ambalo anashikiliwa mjane huyo kumsindikiza ili kuhudhuria mazishi hayo.

Msemaji wa zamani wa Serikali, Muthui Kariuki, maafisa kutoka ubalozi wa Uholanzi, kiongozi wa jeshi, kapteni Kung'u Muigai pamoja na mpwa wa Rais Uhuru Kenyatta, Ngengi Muigai ni baadhi ya watu waliohudhuria mazishi hayo.

Awali mazishi ya bilionea huyo ya bilionea Cohen yaliyopangwa kufanyika jana yalihairishwa hadi jana Jumanne saa 8.30 mchana katika makaburi ya Wayahudi baada ya kukosekana kwa mapadri 10 wa Kiyahudi.

Ilielezwa kuwa waandaji wa mazishi hao walipata mapadri wane kati ya idadi hiyo inayohitajika kwa mujibu wa mila za Kiyahudi.

Mfayabishara huyo aliteka vyombo vya habari nchini Kenya baada ya taarifa za kupotea kwake kuripotiwa polisi kisha mwili wake kupatikana baada ya siku 60.

Bilionea Cohen ambaye alikuwa na umri wa miaka 71 ambaye ni mtaalamu wa utalii na safari kabla ya kifo chake alifungua kesi ya talaka dhidi ya mke wake Saraha. VIDEO:
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad