JKT Tanzania na Mtibwa Sugar Hapatoshi Kesho

KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kesho  uwanja wa Isahmuyo kati ya JKT Tanzania na Mtibwa Sugar, makocha wote wawili wameanza kutumiana tambo kabla ya kukutana uwanjani.

JKT Tanzania na Mtibwa Sugar zote zitakutana zikiwa na machungu ya kupoteza pointi sita za mwanzo kwenye ligi ambapo Mtibwa Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu Zuber Katwila ilipoteza mchezo wa kwanza uwanja wa Samora kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Lipuli na mchezo wa pili mbele ya Simba uwanja wa Uhuru kwa kufungwa mabao 2-1.

JKT Tanzania chini ya Kocha Mkuu, Abdallah Mohamed ‘Bares’ ilipoteza mchezo wa kwanza mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 3-1 na mchezo wa pili ilipoteza ikiwa nyumbani kwa kufungwa bao 1-0 na Lipuli sasa itawakaribisha Mtibwa Sugar.

Bares amesema : ”Tumegundua makosa yetu kwenye michezo iliyopita kwa sasa tunayafanyia kazi mapungufu yetu ili kufanya vema, tunawaomba mashabiki watupe sapoti tunahitaji ushindi hakuna jambo lingine.

Katwila amesema: “Matokeo chanya ndio kitu ambacho tunahitaji, kushindwa kwenye michezo ya nyuuma haina maana kwamba hatuwezi, uwezo upo na makubwa yanakuja, tunahitaji ushindi na inawezekana kwani wachezaji wana morali kubwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad