JPM Aagiza Airbus Nyingine Mbili Mpya


SERIKALI imesaini mkataba wa ununuzi wa ndege mbili aina ya Airbus A220-300 kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).



Mkataba huo umesainiwa jana Alhamisi Septemba 19, 2019, ambapo serikali imewakilishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Benjamin Ndimila. Airbus imewakilishwa na Makamu wa rais wa kampuni hiyo Afrika, Hadi Akoum.



Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Ndimila ambaye hakutaja gharama halisi inayotumika kununua ndege hizo, amesema ndege hizo zitakuwa na tofauti na za aina hiyo ambayo tayari zinatumiwa na ATCL kwani kila kiti kitakuwa na ‘skrini’ “.



Kwa upande wake, Akoum amesema uchongaji wa ndege ya aina hiyo unachukua mwaka mmoja hadi mwaka mmoja na nusu na kwa sasa kuna oda nyingi lakini ndani ya kipindi hicho anatumaini itakuwa imekamilika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad