Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Kamishna Diwani Athuman Msuya mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Kapilimba atapangiwa kazi nyingine.
Kamishna wa Polisi Diwani Athumani aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Septemba 6, 2018, nafasi aliyoitumikia kwa mwaka mmoja na siku 6. Kabla ya kwenda TAKUKURU alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) wa Mkoa wa Kagera.
Nafasi alizoshika Kamishna Diwani Msuya tangu 2015: ⭕️2015: Kaimu Kamishna wa Kamisheni ya Intelijensia ya Jinai
⭕️Mei 2015: Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)
⭕️Nov. 2016: Katibu Tawala Kagera
⭕️Sep. 2018: Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU
⭕️Sep. 2019: Mkurugenzi Mkuu TISS