Kauli ya DPP Kuhusu Kuwaachia HURU Wahujumu Uchumi



Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ofisi yake ipo tayari kutekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli aliyempa siku saba kuzungumza na mahabusu wanaokabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi na endapo wakitubu na kueleza fedha zilipo wasamehewe na kuachiwa huru kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na JAMVI LA HABARI leo Septemba 23 DPP Mganga amesema jambo hilo linawezekana endapo mshtakiwa mwenyewe anatakiwa kuiandikia ofisi yake barua kupitia kwa Mkuu wa Gereza ambapo ametoa muongozo wa namna gani washtakiwa wa uhujumu uchumi wanaosota mahabusu wanatakiwa kufanya ili waachiwe huru.

Amesema mshitakiwa awe tayari na akiri mwenyewe kulipa hasara anayodaiwa ili aachiwe huru; “Utaratibu ni kwamba, mtuhumiwa mwenyewe aliyekuwepo mahabusu anatakiwa aniandikie barua kupitia kwa mkuu wa gereza akikiri kosa na kuomba kutubu haraka iwezekanavyo na sisi tutachukua hatua.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad