Kauli ya Kaseja kabla ya Tanzania kuivaa Sudan leo



Septemba 22 2019 ndio siku ambayo itaanza kutoa picha kwa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ya wachezaji wa ndani, kama wataweza kusonga mbele na kucheza fainali za CHAN 2020 kwa mara ya pili toka wafanye hivyo mara ya kwanza 2009? au bado wanahitaji muda wa kuendelea kujifua zaidi kabla ya kufuzu.

Tanzania Septemba 22 watacheza dhidi ya timu ya taifa ya Sudan na mara ya mwisho 2009 walifuzu kwa kuitoa timu hiyo hiyo, historia itajirudia au vipi? kuelekea mchezo huo leo kocha mkuu na nahodha wa kikosi hicho Juma Kaseja ameongea na waandishi wa habari.

“Kama alivyosema kocha hali ni nzuri kiafya kwa wachezaji tumejiandaa vizuri kwa sababu, kama ilivyokuwa michezo mitatu nyuma na anataka hii timu iende hatua inayofuata, kwa hiyo mimi naamini kwamba mazoezi ambayo tumefanya, marekebisha ambayo tumefanya mchezo wa kesho tutapata matokeo”>>>Juma Kaseja
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad