Mbunge wa Rangwe Ataka Sheria Kuwabana Wanaotoa Ushuzi Ndani ya Ndege



Mbunge wa jimbo la Rangwe nchini Kenya, Dkt. Lilian Gogo anataka itungwe sheria ya kudhibiti watu wanaotoa ushuzi na kuchafua hewa ndani ya ndege.

Akichangia ndani ya Bunge la Kenya, mbunge huyo ameeleza kuwa harufu mbaya ya ushuzi ndani ya chombo hicho husababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na inaweza kuwa chanzo cha kuhatarisha usalama.

Mchango wa mbunge huyo ulizua vicheko na kelele ya muda ndani ya nyumba hiyo ya wawakilishi wa wananchi wa Jamhuri ya Kenya.

“Ushuzi ni chanzo cha usumbufu kwa abiria ndani ya ndege japo hupuuzwa, na ni moja kati ya mambo yanayoweza kuhatarisha usalama, kuna abiria ambao hutoa harufu mbaya na kali baada ya kujamba,” Gogo alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad