Kijana mmoja aelezwa kupofuka kwa kula vibanzi na chips


Wataalamu wanaonya juu ya hatari mbaya za kula vyakula visivyo na virutubisho vya mwili baada ya kijana mmja kupoteza uwezo kabisa wa kuona kwa kuishi kwa kula chips na vibanzi . Madaktari wa macho mjini Bristol walimtibu kijana mwenye umri wa miaka 17-baada ya uwezo wake wa kuona kuwa mbaya hadi kupofuka wanasema.

Tangu alipomaliza masomo yake ya shule ya msingi, kijana huyo amekuwa kila chips, vibanzi na mkate mweupe, au soseji. Vipimo vilionyesha kuwa alikuwa na upungufu mkubwa wa vitamini mwilini na utapiamlo ulio kithiri.

Kijana huyo ambaye alikuwa na umri wa barehe ,ambaye hawezi kutajwa jina, alimuona daktari alipokuwa na umri wa miaka 14 kwasababu alikuwa akihisi kuwa mchovu na anaumwa. Wakati huo alipanikana na tatizo la ukosefu wa vitamini B12 naakapewa tembe za vitamini mbadala, lakini hakuzitumia kama alivyoagizwa au kuboresha lishe yake. Miaka mitatu baadae . alipelekwa katika Hospitali ya macho ya Bristol kwasababu ya kuendelea kupoteza uwezo wa kuona.

Dkt Denize Atan, ambaye alimtibu katika hospitali hiyo anasema “Chakula chake kilikuwa ni cha kununuliwa kwenye maduka ya chipsna samaki wa kukaangwa kila siku . Pia alikuwa akila vibanzi vya dukani aina ya Pringles – na wakati mwingine slesi za mkate mweupe na hakuwahi kula matunda ya aina yoyote ile wala mboga za majani.”Alielezea kuwa hivi ni vyakula ambavyo hakuweza kuvivumilia kabisa, na kwa hiyo chips na vibanzi ni aina pekee za vyakula ambavyo alivitaka na kuhisi kuwa angeliweza kuvila .”


Dkt Atanna na madaktari wenzake walimfanyia tena vipimo vya viwango vya vitamini na kubaini kuwa alikuwa ana upungufu mkubwa wa vitamini B12 pamoja na vitamini nyingine na madini mwilini kama vile madini ya chuma na vitamini D.


Matokeo yake: Hakuwahi kuwa na uzito wa chini wa mili, lakini alikuwa na utapiamlo mkubwa kutokana na kula chakula kisichofaa bila mpangilio. “Alikuwa amepoteza madini katika mifupa yake, jambo ambalo lilikuwa ni la kutisha sana kwa kijana mdogo wa umri wake .” Alipewa tembe za vitamini mbadala na kushauriwa kumuona mtaalamu wa lishe na timu ya wataalamu wa afya ya akili. Kuhusu kupoteza uwezo wa kuona, alifikia kiwango cha kusajiliwa kama kipofu. “Alikuwa na alama za upofu katikati mwa macho yake ,” alisema Dkt Atan. ” Hii ina maana kuwa hawezi kuendesha gari na itakuwa ni vigumu kwake sana kusoma , kutazama televisheni au kutambua sura za watu. “Anaweza kutembea nje mwenyewe kwasababu ana uwezo mdogo sana wa kuona.”

Kwa mujibu wa BBC. Hali ya kiafya aliyonayo kijana huyo inayofahamika kwa lugha ya kitaalamu kama Nutritional optic neuropathy – inatibiwa ikiwa itabainika mapema .Ukiachwa kwa muda mrefu , hata hihvyo mishipa ya neva iliyopo katika jicho huhfa na kuharibika kabisa. Dkt Atan alisema anashukuru kuwa visa kama hivi zio vya kawaida, lakini wazazi wanapaswa kujua uwezekano wa madhara yanayoweza kusababishw ana kuchagua chakula kwa watoto na kwamba wanahitaji usaidizi wa kitaalamu. Rebecca McManamon, daktari wa lishe na msemaji wa shirika la Uingereza la lishe anasema kuchagua chakula kunaweza kusababishwa na sabanbu mbali mbali ,kama vile ulaji wa vyakula fulani, , mzio (allergies) na kudumaa kwa ubongo( autism) na hali hiyo inahitaji tathmini ya daktari bingwa. “Ni muhimu kutambua kuwa tangu mwaka 2016 serikali ya Uingereza ilishauri kila mtu awe anachukua tembe mbadala ya vitamini D kati ta mwezi Oktoba na Machi, kwasababu ni vigumu kupata vyakula vyenye vitamini hiyo nchini uingereza wakati huo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad