Kikongwe Aliyepigania Ardhi yake Aanza Kulipwa Mamilioni



Hatimaye Bibi Nasi Muruo (98) mkazi wa eneo la Sinoni, jijini Arusha ameanza kupokea fidia ya ardhi yake kwa kulipwa kiasi cha Sh69.1 milioni kati ya Sh519.3 milioni anazopaswa kulipwa.

Fedha hizo zimetolewa na Kanisa la Evengalistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) baada ya kuhangaikia kusaka haki yake kwa miaka 42.

Serikali ya Tanzania imezipa miezi mitatu kaya 110 zilizojenga kwenye ardhi ya kikongwe huyo kumlipa Sh519.3 milioni kutokana na ardhi ambayo inamilikiwa na kila kaya.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Bibi Muruo alimshukuru Rais wa Tanzania, John Magufuli, Waziri wa Ardhi wa nchi hiyo, William Lukuvi kwa kumsaidia kupata haki yake.

“Naishukuru sana Serikali, leo nimeanza kupata haki yangu, baada ya kuitafuta kwa miaka 42, nitakula nyama leo,” amesema

Katibu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Askofu Leonard Mwizarubi amesema kanisa hlo limeamua kumlipa kiasi chote cha fedha bibi huyo ili aweze kuishi maisha mazuri.

“Kanisa lina eneo la mita za mraba la 3,458 na kulingana na maagizo ya serikali, gharama yake ni Sh69.160,000 milioni na tumelipa zote ili bibi apate haki yake akiwa hai, ili ikiwezekana aweze kujenga nyumba yake” alisema

Askofu Mwizarubi amesema kanisa limelipa fedha hizo kutekeleza maagizo ya Serikali kwa kuamini bibi huyo alikuwa na haki zote za umiliki wa eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad