Kikosi cha Yanga kimeondoka leo kwenda Zambia kwaajili ya mchezo wa marudiano na Zesco United unaotarajiwa kufanyika Ijumaa, Septemba 27, katola Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola ikiwa ni hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga inatakiwa kushinda ugenini baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita Septemba 14.
Huku Azam FC inayowakilisha katika michuano ya Kombel la Shirikisho Afrika ikiwa imeweka kambi jijini Harare, Zimbabwe tayari kwaajili ya mchezo wao utakaofanyika huko Bulawayo dhidi ya Timu ya TriAngle.