Kilichojiri Kesi ya Madawa ya Shamim Mwasha na Mumewe


UPANDE wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi inayomkabili Blogger, Shamim Mwasha(41) na mumewe, Abdul Nsembo (45) bado haujakamilika hivyo kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kusikilizwa.



Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi, Kelvin Mhina wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa. Wakili Wankyo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo anaomba ahirisho la kesi hiyo.



Hata hivyo, upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Charles Kisoka umeomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi huo. Katika majibu yake Wakili Wankyo amedai watajitahidi kuharakisha upelelezi huo.



Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mhina ameutaka upande wa mashtaka kama ambavyo wakili wa utetezi ameomba upelelezi huo ufanyike haraka ili kesi hiyo iweze kuendelea kwa wakati na hakimu ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11 mwaka huu.



Washtakiwa wamerudishwa rumande na washtakiwa hao wanatuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya, Mei 1, 2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad