Kilichomuua Mugabe chafichuliwa na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
0
September 24, 2019
Serikali nchini Zimbabwe imefichua kuwa rais wa zamani nchini humo Robert Mugabe amefariki kutokana na saratani.
Serikali imeeleza kwamba matibabu ya chemotherapy anayepatiwa mgonjwa wa saratani kupunguza sumu mwilini yalisitishwa wakati ilipodhihirika kuwa hayasaidii tena.
Mugabe alifariki mapema mwezu huu nchini Singapore akiwa na umri wa miaka tisaini na tano.
Anatarajiwa kuzikwa katika kaburi kwenye eneo la kitaifa la kuzikwa mashujaa ambalo linajengwa mjini Harare.
Ni sehemu ambapo wapiganiaji uhuru wengi nchini humo walio maarufu wamezikwa.
Enzi ya kisiasa ya Mugabe
Ikiwa ni mara ya kwanza kufichuliwa kwa chanzo cha kifo cha kiongozi huyo wa zamani nchini, rais Emmerson Mnangagwa amenukuliwa na vyombo vya habari akiwaambia wafuasi wa chama tawala Zanu- PF mjini New York, ambako amekwenda kuhudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa, kuwa Mugabe alikuwa na saratani, lakini hakufichua ni saratani ya aina gani.
“Matibabu yalisitishwa, madaktari walikatiza matibabu, chemotherapy, moja, kwasababu ya umri wake na pia kwasababu saratani yake ilikuwa imesambaa na matibabu yalikuwa hayasaidii tena,” Mnangagwa alisema katika matamshi yaliochapishwa kwenye gazeti la The Herald leo Jumatatu.
Mugabe(kulia) akiwa na Nkomo (kushoto kwake)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRobert Mugabe(kulia) akiwa na Joshua Nkomo (kushoto kwake)
Urithi wa utawala wake Robert Mugabe
Kwa kadri miaka yake ilivyozidi kuongezeka huku na matatizo ya kiafya pia yakizidi kuongezeka yalileta minong’ono ya nani wa kuichukua nafasi yake.
Lakini fitna ziliendelea kufanyika kwa wale walioonekana wanaweza kuchukua nafasi ya yake na hivyo kuthibitisha namna uongozi wa Zimbabwe unashikiliwa na Mugabe pekee.
Na hata Mugabe alionekana kuvunja nguvu ya utawala wowote uliokuwa kinyume nae.
Kufuatia uvumi wa mkewe Grace kutaka kutawala pale mume wake atakapofariki akiwa madarakani Mugabe alitangaza nia yake ya kugombea tena mwaka 2018 ambapo angekuwa na umri wa miaka 94.
Na katika kuondoa maswali yaliyokuwa yamebaki kati ya wale waliokuwa wakidhaniwa huenda wangekuwa warithi, mwezi Februari Mugabe alitangaza rasmi kuwa ataendelea kuwa madarakani mpaka pale Mungu atakapomuita.
Kufuatia tukio hilo haikuwa tena Mungu ila ni umoja wa majeshi wa Zimbabwe ndiyo yaliyomuita Mugabe.
Mnamo mwezi Novemba 2017 aliwekwa kizuizini kwa siku nne huku aliyekuwa makamo wake Emmerson Mnangagwa akichukua nafasi yake kama kiongozi wa Zanu-PF.
Novemba 21 spika wa bunge la Zimbabwe alitangaza rasmi kujiuzulu kwa raisi Mugabe baada ya muda mrefu kukataa kibabe kufanya uamuzi huo.
Mugabe alifikia makubaliano ya kupata ulinzi kwake na familia yake kutokana na hofu ya kuuawa na kuendeleza biashara yake. Pia alipatiwa nyumba, wafanyakazi, usafiri na hadhi yake ya kidiplomasia.
Kama ilivyo tabia yake ya kutopenda anasa Robert Mugabe alivaa kawaida na hakutumia kilevi.
Mtu ambaye alikua akitukuzwa kama mshindi katika mapigano ya Afrika kuushinda ukoloni amegeuka kuwa dikteta, akikiuka haki za binadamu na kugeuza nchi ambayo ilikuwa ni yenye utajiri
Mchango wake utaendelea kukumbukwa miaka na miaka.
Chanzo BBC.
By Ally Juma.
Tags