Kiongozi wa Upinzani Rwanda FDU-Inkingi Auawa kwa Kuchomwa Kisu


Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Rwanda amedunguwa kisu na kuuawa, chama chake cha FDU-Inkingi kinasema.

Syridio Dusabumuremyi, mratibu wa chama hicho cha upinzani FDU-Inkingi, alikuwa kazini wakati aliposhambuliwa na wanaume wawili, kiongozi wa chama hicho Victoire Ingabire ameieleza BBC.

Mwanamume huyo ambaye ni baba ya watoto wawili alikuwana duka la kuuza chakula katika kituo cha afya katika wilaya ya kati ya Muhanga.

Raia mwingine wa Rwanda auawa uhamishoni
Bi.Ingabire avilaumu vyombo vya usalama Rwanda
Je upinzani una makali kiasi gani Afrika ?

Idara ya upelelezi nchini Rwanda imetuma ujumbe katika mtandao wa twitter kueleza kwamba imewakamata washukiwa wawili wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya Syridio Dusabumuremyi.

Kwenye ujumbe uliofuata, idara hiyo ya upelelezi imeeleza kwamba katika uchunguzi wa awali, washukiwa wawili wamekamatwa kwa kuhusika na mauaji hayo.

Imeendelea kusema uchunguzi unaendelea kubaini dhamira ya mauaji hayo.

Bi Ingabire anasema mauaji ya Dusabumuremyi ni ya hivi karibuni kufuatia msururu wa mashambulio dhidi ya wafuasi wa chama chake kwa lengo la kuwatishia.

Miezi miwili iliyopita, Eugène Ndereyimana, mwakilishi wa chama cha FDU-Inkingi kutoka eneo la mashariki mwa Rwanda alitoweka. Mpaka sasa hajapatikana.

Mnamo Machi, Anselme Mutuyimana, msemaji wa chama hicho alitekwa na baadaye kukutikana amefariki msituni magharibi mwa nchi hiyo.

Mnamo 2016, mwanachama wa FDU-Inkingi Jean Damascène Habarugira aliuawa.

Bi Ingabire, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa rais Paul Kagame, amesema chama chake kinalengwa kwasababu kinapania kutetea haki za raia wa Rwanda na uhuru wao.

"Lengo letu ni zuri na hatutaacha kulipigania hata wakafanya lolote," amesema
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad