Wanaume wawili Waislamu nchini Marekani wametaka uchunguzi kufanywa baada ya kusema kwamba walibaguliwa kidini katika ndege moja iliokuwa ikielekea mjini Dallas.
Kampuni ya ndege ya American Airline ilisema kwamba walisitisha ndege hiyo kufuatia ‘wasiwasi uliotolewa na wafanyakazi na abiria’.
Abderraoof Alkhawaldeh na Issam Abdallah wamedai kwamba safari yao ilifutiliwa mbali kwa kuwa abiria hawakufurahia kusafiri na wanaume hao wenye imani ya dini ya Kiislamu.
Kiongozi wa dini, Abderraoof Alkhawaldeh (kulia) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari
Taarifa ya kampuni hiyo ya ndege ilisema kuwa wasiwasi uliowakabili abiria wa ndege hiyo ulisababisha kufutiliwa mbali kwa safari ya wawili hao mara tu baada ya kusalimiana kwa kupungiana mikono.
”Marekani na washirika wake wote wana jukumu la kutilia maanani usalama na wasiwasi wa kiusalama wa wafanyakazi na abiria” , ilisema katika taarifa.
Ni nini kilichotokea katika ndege?
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Aljazeera na BBC, Bwana Alkhawaldeh na bwana Abdallah walitoa madai hayo katika mkutano na vyombo vya habari ulioandaliwa na baraza la uhusiano wa Waislamu wa Marekani na kutangazwa katika mtandao wa Facebook.
Mnamo tarehe 14 mwezi Septemba, wanaume wote wawili waliorodheshwa miongoni mwa abiria watakaosafiri kutoka Birmingham , Alabama kuelekea Dallas Texas katika ndege ya kampuni ya Marekani inayoendeshwa na kampuni ya ndege ya Mesa Airlines.
Imam Omar Suleiman (center) said airports are "a scary place for Muslims," as racial profiling instances increase.
Walikuwa wakisafiri kila mtu kivyake, lakini wakatambuana kupitia kundi moja la Kiislamu na kupungiana mikono wakiwa ndani ya ndege.
Mtangazaji mmoja alisema kwamba ndege hiyo ilicheleweshwa na bwana Abdallah akaelekea msalani.
Alipotoka mfanyakazi mmoja wa ndege alikuwa amesimama nje ya choo hicho kama ambaye alikuwa akijaribu kusikiliza kilichokuwa kikiendelea ndani.
Muda mfupi baadaye wafanyakazi hao waliambia abiria kwamba safari hiyo ilifutiliwa mbali na kwamba walipaswa kutoka katika ndege hiyo.
Bwana Alkhawaldeh alisema alisikia mfanyakazi mmoja akimwambia abiria hatua hiyo ilikuwa ya kiusalama.
Baada ya kutoka wawili hao wanasema kwamba walifuatwa na mtu aliyekuwa amevalia nguo za raia , maafisa waliovalia sare za kazi na baadaye na maafisa wa Ujasusi wa FBI.
Aajenti mmoja alimchukua bwana Abdallah katika chumba kimoja cha faragha na kudai kumuuliza jina lake na kazi anayofanya na kusema kwamba mzigo wake utalazimika kukaguliwa tena.
Alipouliza ni nini kilichokuwa kikiendelea , ajenti huyo alidai kwamba wafanyakazi wa kampuni hiyo ya ndege waliwaita maafisa wa polisi na kusema kwamba hawakuridhika kusafiri naye.
Sababu iliotolewa na ajenti huyo ni kwamba bwana Abdallah aliingia msalani na kupiga maji mara mbili.
Kulingana na bwana Abdalla ajenti huyo baadaye aliomba msamaha na kumwambia kwamba anaweza kwenda kupanda ndege yake .
”Nilihisi kwamba walikuwa wanabagua kabila langu na dini yangu” , alisema bwana Abdallah.
Abiria wote baadaye walisafiri katika ndege iliofuata isipokuwa wawili hao