Klabu za Uingereza zatawala orodha ya wachezaji walioteuliwa katika kikosi bora cha FIFA
0
September 06, 2019
Ligi ya Uingereza ina idadi kubwa ya wachezaji waliochaguliwa kuorodheshwa miongoni mwa kikosi bora cha Fifa cha wachezaji 11 katika kipindi cha miaka kumi.
Wachezaji 21 kati ya 55 walioteuliwa wanacheza soka yao ya kulipwa nchini England huku ligi hiyo ya Premia ikimaliza utawala wa ligi ya la Liga .
Wachezaji saba wa klabu ya Liverpool walioshinda ubingwa wa Ulaya wwameorodheshwa miongoni mwa wale watakaowania nafasi hizo 11 za kikosi cha Fifa ijapokuwa Real Madrid na Barcelona wana wachezaji wengi zaidi.
Kikosi hicho cha wachezaji saba 11 kitafichuliwa katika tuzo bora za Fifa mjini Milan tarehe 23 Septemba.
Zaidi ya wachezaji 23,000 wa kulipwa duniani walitakiwa kuchagua kikosi bora na Fifpro, Muungano wa wachezaji kutokana na kiwango cha mchezo wao kati ya tarehe 18 Julai 2018 na Julai 2019.
Walinda lango: Alisson Becker (Liverpool), David De Gea (Manchester United), Ederson Moraes (Manchester City), Jan Oblak (Atletico Madrid), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona)
Mabeki: Jordi Alba (Barcelona), Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Daniel Alves (Paris St-Germain/Sao Paulo), Joao Cancelo (Juventus/Manchester City), Daniel Carvajal (Real Madrid), Giorgio Chiellini (Juventus), Virgil van Dijk (Liverpool), Diego Godin (Atletico/Inter Milan), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Kalidou Koulibaly (Napoli), Aymeric Laporte (Manchester City), Matthijs de Ligt (Ajax/Juventus), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Andrew Robertson (Liverpool), Alex Sandro (Juventus), Thiago Silva (Paris St-Germain), Raphael Varane (Real Madrid), Marcelo (Real Madrid), Kyle Walker (Manchester City)
Viungo wa kati: Sergio Busquets (Barcelona), Casemiro (Real Madrid), Kevin de Bruyne (Manchester City), Christian Eriksen (Tottenham Hotspur), Frenkie de Jong (Ajax/Barcelona), Eden Hazard (Chelsea/Real Madrid), N'Golo Kante (Chelsea), Toni Kroos (Real Madrid), Arthur Melo (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Paul Pogba (Manchester United), Ivan Rakitic (Barcelona), Bernardo Silva (Manchester City), Dusan Tadic (Ajax), Arturo Vidal (Barcelona)
Washambuliaji: Sergio Aguero (Manchester City), Karim Benzema (Real Madrid), Roberto Firmino (Liverpool), Antoine Griezmann (Atletico/Barcelona), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Sadio Mane (Liverpool), Kylian Mbappe (Paris St-Germain), Lionel Messi (Barcelona), Neymar (Paris St-Germain), Cristiano Ronaldo (Juventus), Mohammed Salah (Liverpool), Son Heung-min (Tottenham Hotspur), Raheem Sterling (Manchester City), Luis Suarez (Barcelona)
Tags