Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Rugby ya Wales Rob Howley amerudishwa nyumbani kutoka kambi ya Kombe la Dunia ya timu yake iliyokuwa inajiandaa michuano ya Kombe la Dunia Rugby kwa tuhuma za kujihusisha na ubashiri (bettting).
Inafahamika kuwa Rob Howley alibashiri (betting) mechi za Rugby (Rugby Union Matches) amesimamishwa kujihusisha na masuala yoyote ya mchezo wa Rugby na atakumbana adhabu ya kufungiwa kwa kukiuka kanuni ambapo haziruhusu wahusika wa michezo (wachezaji, makocha na viongozi) kushiriki kubeti kwani wanaweza kupelekea kupanga matokeo.
Rob Howley anaondoka katika kambi ya timu ya taifa ya Wales zikiwa zimesalia siku siku sita kabla ya kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Georgia katika michuano hiyo kombe la Dunia Japan, nafasi ya Rob Howley itarithiwa na kocha Stephen John hadi 2020.