Kocha Stars: Tupo Tayari Kuwakabilo Wasudani


JUMA Mgunda, Kaimu Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania inayojiaandaa na mchezo wa kimataifa wa michuano ya Chan dhidi ya Sudan amesema kuwa hakuna wapo tayari kupata ushindi.

Stars kwenye michuano hii ya wachezaji wa ndani itarusha kete yake ya kwanza Jumapili na tayari timu imeanza maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa wachezaji wanatambua kazi yao kubwa ni kutafuta matokeo na wapo tayari kwa hilo.

“Mapungufu ambayo yalikuwepo awali hasa kwenye safu ya ushambuliaji ndiyo tunayafanyia kazi kwa ukaribu kwani ili timu ishinde ni lazima ipate mabao mengi kwa kuwa tunaanza nyumbani basi tunapambana kupata matokeo chanya,” amesema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad