Kortini Akijifanya Usalama wa Taifa Amsaidie Malinzi

THOMAS Mgoli (37), mkazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam amepandishwa kizimbani katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za kujifanya Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ili amsaidie aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, katika kesi yake ambayo bado anasota mahakamani.



Katika kesi hiyo namba namba 98 ya mwaka 2019, iliyosomwa leo Septemba 20, 2019, na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina, Mgoli amesomewa mashtka matatu.



Shtaka la kwanza anatuhumiwa kwa kujifanya ofisa wa TISS, kosa ambalo alilitenda kati ya Desemba 1, 2017 na Agosti 2019, katika eneo la Mahabusu ya Keko.



Katika shtaka la pili, Mgoli anatuhumiwa kujiingizia pesa kwa njia ya udanganyifu ambapo Agosti 17, 2019 na 29 Agosti 2019 alijipatia kiasi cha Tsh. 280,500 kutoka kwa Lucy Ngongoseki akiwa eneo la Mahabusu ya Keko akijifanya Ofisa Usalama ambaye alidai atamsaidia kwenye kesi namba 213 ya mwaka 2017 inayomkabili Jamali Malinzi ya uhujumu uchumi inayomkabili Jamal Malinzi.



Katika Shtaka la tatu mtuhumiwa anadaiwa kufanya utakatishaji fedha haramu katika tarehe 17 Agosti 2019 na 29 Agosti 2019 akitumia pesa kiasi Tsh 280,500 ilhali alijiua ni zao la kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.



Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu Mhina alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpatia mshitakiwa dhamana, pia haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi, hivyo mshtakiwa atakwenda rumande. Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, ambapo kesi imeahirishwa hadi Oktoba 4, 2019.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad