Kuna upotevu wa zaidi ya Bilioni 120 vyama vya ushirika - Bashe
0
September 27, 2019
Naibu Waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi ya shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), wamebaini kuwepo kwa upotevu wa jumla ya shilingi Bilioni 123 kwenye vyama vya ushirika.
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa bodi ya pamba nchini kinachofanyikia kwenye ukumbi wa benki kuu (BOT) jijini Mwanza ambapo ameeleza kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua kali.
“Hapa nina kabrasha, nitawapatia wakuu wa mikoa wote na nitamkabidhi kiongozi wa tume, kwa ripoti ya COASCO ushirika kumetokea jumla ya upotevu wa sh. Bilioni 123, na nisema hapa hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika wote,” amesema.
“Hizi ni pesa za wakulima, wote waliohusika katika huu upotevu watachukuliwa hatua kali na wakuu wa mikoa tutawapa majina ya Amcos gani wanahusika na mnatakiwa kuchukua hatua,” amesema Bashe.
Aidha ameongeza kuwa ushirika uliopo kwa sasa unahitaji mabadiliko makubwa kwani hauwezi kutatua matatizo ya kilimo hasa kwenye zao la pamba, ambapo mfumo unatakiwa kubadilishwa kutoka ushirika wa kuhudumia wakulima na kuwa ushirika wa kibiashara
Tags