Kuweni makini na mnaowasikiliza - Rais Magufuli


Rais John Magufuli amewataka watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi walioagizwa kuwasilisha barua zao za kuomba msamaha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) waamue wanamsikiliza nani kati ya Mawakili wanaotaka kuwachomoa pesa au DPP.

Ametoa kauli hiyo leo , alipokuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kusamehe watuhumiwa hao wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali.

“Msamaha ukishautoa ni msamaha la sivyo wewe uliyetoa utaibeba hiyo dhambi kwa Mungu, ninafahamu wapo wanaodanganywa na mawakili wao ili waendelee kuwachomoa pesa wanaawambia ukiomba msamaha maana yake unakuwa umeshajishtaki mwenyewe sasa hiyo ni shauri yao waamue wanamsikiliza nani,” amesema Magufuli.

Aidha ameitaka ofisi ya DPP kuharakisha juu ya suala hilo ili watuhumiwa hao waweze kutoka wakajumuike na familia zao kutokana na sababu kuwa waliingia kwa njia ya mahaka hivyo wanapaswa kutoka kwa njia ya mahakama hivyo wawafikishe kwenye vyombo vya sheria ili waweze kuachiwa.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ningeomba, Hii clip ipelekwe Na waione na kuisikia wanao kabiliwa na hizi kesi nchi nzima Leo Leo, Mkuu wettu wa nchi amesema Nini na ana msimamo gani juu ya kuurudisha Furaha kwa Familia naUjenzi wa Maendeleo ya Nchi.

    Mungu Akubariki kipenzi chetu JPJM.

    ReplyDelete
  2. Ningeomba, Hii clip ipelekwe Na waione na kuisikia wanao kabiliwa na hizi kesi nchi nzima Leo Leo, Mkuu wettu wa nchi amesema Nini na ana msimamo gani juu ya kuurudisha Furaha kwa Familia naUjenzi wa Maendeleo ya Nchi.

    Mungu Akubariki kipenzi chetu JPJM.

    ReplyDelete
  3. Ningeomba Magerezani Wa facilitate Runinga, Hii clip ipelekwe Na waione na kuisikia wanao kabiliwa na hizi kesi nchi nzima Leo Leo, Mkuu wettu wa nchi amesema Nini na ana msimamo gani juu ya kuurudisha Furaha kwa Familia naUjenzi wa Maendeleo ya Nchi.

    Mungu Akubariki kipenzi chetu JPJM.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad