Kwa mara ya kwanza wanasayansi wagundua maji kwenye sayari ya mbali
0
September 13, 2019
Kwa mara ya kwanza wataalamu wa anga wamegundua maji katika sayari inayozunguka katika nyota iliyoko orbiti yenye mazingira sawa na yaliyo duniani.
Utambuzi huo unaifanya dunia inayotambulika kwa lugha za kisayansi K2-18b kua ni moja ya sehemu zitakazofanyiwa utafiti juu ya viumbe wanaoaminika kuwepo duniani 'aliens'.
Ndani ya miaka kumi kuanzia sasa, darubini mpya ina uwezo wa kutambua kama anga za sayari K2-18b ina gesi ambazo zina uwezekano kua zilitokana na viumbe hai.
Taarifa hizo zimeandikwa na jarida la kisayansi la 'Nature Astronomy'.
Prof. Giovanna Tinnetti, mwanasayansi aliyeongoza watafiti kutokea chuo cha London (UCL),ameeleza kuwa ugunduzi huo ni mkubwa.
"Hii ni mara ya kwanza kwa maji kugunduliwa kwenye sayari yenye hali sawa na dunia, katika nyota hii ambayo hali ya hewa yake ni rafiki kwa maisha ya viumbe hai"Profesa alifafanua.
Sayari hii mpya ina ukubwa mara mbili ya dunia na katika kundi lake inajulikana kama "Super Earth" na ina hali ya hewa inayoweza kuruhusu maji au kimiminika kuanzia nyuzi joto sifuri mpaka.
Sayari ya K2-18b yenye umbali wa maili millioni 650 kutoka duniani ni miaka 111 kwa spidi ya mwanga, hivyo ni ngumu kutuma kifaa huko
Hivyo nafasi pekee ya kuitambua zaidi ni kusubiri kwa kizazi kijacho cha wana anga kuitambua zaidi sayari hiyo hasa kwa darubini mpya itakayozinduliwa kuanzia miaka ya 2020.
Timu ya wanasayansi iliyogundua ilipitia sayari zilizogunduliwa na Hubble Space Telescope kati ya mwaka 2016 na 2017 na ndipo walipoigundua K2-18b kuwa ina uwezo wa kuwa na maji.
Wana-anga wengine wanapingana na taarifa hiyo juu ya uwezekano wa viumbe wengine kuishi.
Tags