Laini za simu milioni 2 pekee ndizo zimesajiliwa kwa alama za vidole kati ya Milioni 44
0
September 19, 2019
Laini za simu milioni 5.2 ndio zimesajili kwa alama za vidole ikiwa imesalia miezi mitatu kabla ya kukamilika kwa usajili huo. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 12 pekee ya laini zote za simu zinazotumika nchini Tanzania.
Akizungumza leo mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Frederick Ntobi amesema hadi Agosti, 2019 laini milioni 5.2 ndio zimesajiliwa kati ya milioni 44.2.
“Tunasisitiza baada ya Desemba 31, 2019 laini zote zitakazokuwa hazijasajiliwa kwa alama za vidole hazitaruhusiwa kutumika kwenye mitandao ya simu,” amesema Ntobi.
Kufuatia hilo watoa huduma za mawasiliano nchini wameanzisha kampeni ya uhamasishaji inayolenga kuwahamasisha watumiaji wa simu kusajili laini zao.
Kampeni hiyo inayoratibiwa TCRA imezinduliwa leo Alhamisi Septemba 19, 2019 kwa kuzihusisha kampuni zote za simu nchini.
Tags