Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kanda ya ziwa kwa kushirikiana na mamlaka ya vitambulisho NIDA pamoja na watoa huduma za mawasiliano ya simu wameanzisha kampeni maalumu ya kufanya usajili wa laini za simu kwa njia za vidole.
Kampeni hiyo inatarajiwa kuanza Septemba 30, 2019, mkoani Mwanza eneo la Rock City Mall ambapo itenda kwa jina la mimi nimesajili namba yangu ya simu wewe unangoja nini?, kampeni hiyo inatarajiwa kufanywa kwa kipindi chote hadi pale zoezi la usajili litakapositishwa mnamo Disemba 31, 2019.
Akizungumza leo Septemba 27, 2019 Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano, Mhandisi Francis Mihayo, amewaomba wananchi kuhakikisha wanafanya zoezi hilo mapema ili kuondokana na usumbufu utakaojitokeza mwishoni mwa zoezi hilo.
Amesema ambao hawatasajili laini zao hadi ifikapo Disemba 31, 2019, zitasitishwa kutoa huduma zote ikiwa pamoja na kupiga na kupokea simu.
Aidha, Afisa wa NIDA, Raphael Manase amesema kuwa watakwepo katika usajili huo ambapo wameongeza wigo mpana zaidi kwa mwananchi kuweza kujua namba zao za usajili wa vitambulisho vyao vya taifa kulingana na mahali walipo.
Ambapo ametoa hatua kuu tatu ambazo mtu anaweza kutumia ili kuweza kupata namba yake ya usajili kama alishasajiliwa awali
”Hatua ya kwanza unayoweza kufanya kupata namba yako ya usajili wa kitambulisho cha Taifa ni kwenda Serikali ya Mitaa, au serikali ya vijiji namba zimeenda kwa uongozi wa serikali za mitaa na serikali za kijiji’, mbili unaweza kupata hizo namba kwa njia ya simu kwa kupiga *152*00# au kutembelea tovuti yetu ya NIDA ambayo unaweza kuinga pale kwa kuandika www.nida.go.tz kuna sehemu imeandikwa kitambulisho cha taifa, kuna option mbili kwanza kujua namba ya kitambulisho pili kupata kopi ya kitambulisho ambapo kuna maswali utaulizwa ili kuthibitishwa” amesema Manase
Ameongezea kuwa Kwa wale ambao bado hawajasailiwa wanasahuriwa kufika ofisi za NIDA ili kusaidiwa zaidi.
Laini za Simu Zisizosajiliwa kwa Alama za Vidole Kuzimwa Ifikapo Desemba 30
0
September 28, 2019
Tags