Waliosombwa na mafuriko ni watalii sita raia wa Kenya na mtu mmoja raia wa kigeni. Shughuli za kuwatafuta watu hao zimekuwa zikiendelea usiku kucha na tayari miili mingine miwili imeopolewa kutoka kwenye maji.
Shirika la habari la AFP linaripoti kuwa watu hao walikuwa miongoni mwa kundi la watu 12 waliokuwa wanazuru hifadhi ya Hells Gate, karibu kilomita 100 Kaskazini magharibi mwa Jiji kuu la Nairobi.
Vyombo vya habari nchini Kenya vianripoto kuwa manusra waliwafahamisha maafisa wa hifadhi hiyo kuhusu tukio hilo ndipo shughuli za kuwatafuta wahasiriwa zikaanzishwa mara moja.
Afisa wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia shirika la Habari la AFP kuwa watu waliosombwa na mafuriko hayo na ambao hawajapatikana huenda ”wamefariki” kutokana na ushahidi uliotolewa na wale walionusurika mkasa huo.
Hifadhi ya Hell’s Gate, limepewa jina hilo kutokana na vyanzo vyembamba vya maji yanayopita kati kati ya milima na ambayo husababisha mafuriko.
Eneo hilo linasifika kwa mandhari yake ya kupendeza ambayo pia imeangaziwa katika filamu ya The Lion King. Hifadhi ya hiyo iliyobuniwa mwka 1984, pia ina vituo vitatu vya kukuza kawi ya mvuke