Lissu Sijakuonea Umeyataka Mwenyewe- Ndugai

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amesema Mbunge Miraji Mtaturu, ni mbunge halali wa Singida Mashariki, kwa mujibu wa sheria baada ya mbunge wa awali, Tundu Lissu, kuvuliwa ubunge kutokana na kukiuka taratibu za kisheria.



Spika amewataka wabunge kuwa na nidhamu na kufuata taratibu za bunge ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa na kuomba udhuru inapotokea wanaumwa au la.



Mapema leo, Mahakama Kuu Kanda ya Dar  es Salaam , imetupilia mbali maombi ya Tundu Lissu kupinga uamuzi wa Ndugai kumvua ubunge kwa maelezo kuwa alipaswa kuweka pingamizi dhidi ya uchaguzi na si kuomba mahakama ibatilishe uamuzi wa spika.



Jaji Matupa amesema, hawezi kufanya maamuzi ya kufuta uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa sababu ataingia kwenye mgogoro wa kikatiba na mhimili wa bunge.



Akiendelea kufafanua, Jaji Matupa amesema, endapo maombi hayo ya Lissu yakisikilizwa mpaka mwisho na Lissu akashinda kesi hiyo, Jimbo la Singida Mashariki litalazimika kuwa na wabunge wawili (yaani Tundu Lissu na Miraji Mtaturu) kwa wakati mmoja.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera Utawala wa sheria.
    Hongera Tanzania.
    Hongereni wana Singida Mashariki kwa uchaguzi wenu Sahihi na kupata mchapa kazi wa kutatua Adha zenu na kuleta chachu ya Maendeleo Jimboni.

    Wajenga Mazingira ya Ukimbimzi imekula kwao.Na vibaraka wenzao. Ndege yetu imerudi Salama Salmini.

    Hati yako ya maombi ya dharura imepata uamuzi sahihi.

    Tumechukia Hewa Hewa na sasa kwamara ya kwanzaKulikuwa na Mchakato wa kutuletea Mwakilishi Hewa ila wawakilishwaji huko Ikungi Wamekushtukia. Kwani alizeti si unaweza kulima au niimwambie Msando/ Manyama wakupe hata ukalani?

    Chamani usithubutu kumtikisa m/kiti
    muuulize jitto ruyagwa wa Uvira kilimtokea nini akujuze.

    Agwe Ndugai.. To unyamale Mwaha..Hawa wapotoshaji ni level ya chini yetu na kina Bwakila na Pwaguzi.

    Nyie endeleeni kujenga nchi na Maendeleo. wacheleweshaji hawana Dili
    tena.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad