Lowassa Ammwagia SIFA Rais Magufuli....Kasema Utendaji kazi Wake Umeifanya Nchi Ishike Adabu


Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Lowassa amepongeza utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli ambapo amesema kampeni yakutumbua watu ambao ni wazembe imesaidia nchi kushika adabu na mambo yanakwenda kwa utaratibu

Lowassa ameyasema hayo jana  katika mahafali ya shule ya msingi ya Meyers mjini Arusha.

"Rais  Magufuli anastahili pongezi anafanya kazi nzuri sana, tunaona mawaziri wanafanya kazi nzuri , Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) yupo kule wengine huku, nchi imewaka moto kila sehemu.” Amesema Lowassa

Kwa mujibu wa Lowassa, kazi za Rais Magufuli, zinatakiwa kupakwa ‘poda’ kwa kuhusisha uboreshaji wa elimu ambayo itawapa ujuzi wahitimu kujiajiri.

"Kuna vijana wengi wanamaliza masomo kutokana na mpango wa elimu bure sasa tujitahidi elimu hii iwasaidie vijana kupata ujuzi na ubunifu ili kuweza kujiajiri."Ameongeza Lowassa.

Lowassa aliyejiunga ndani ya Chadema tarehe 28 Julai 2015 na kupitishwa kuwa mgombea urais wa chama hicho akiungwa mkono na vyama rafiki vya Ukawa, alishindwa kuhimili mikikimikiki ya upinzani na kuamua kurejea ndani ya chama tawala CCM tarehe mosi Machi mwaka huu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad