Maghembe Aitaka Serikali Kuingilia Kati Wizi wa Vifurushi vya Simu, ‘Vodacom sio Vizuri…’


Mbunge wa Mwanga (CCM), Jumanne Maghembe ameilalamikia mitandao ya kijamii na kuionya tabia ya kuwaibia wateja wao pesa pindi wanapojiunga na vifurushi vyao.

Akizungumza hayo ametolea mfano mtandao anaotumia yeye wa Vodacom kuwa umekuwa ukimuibia sana dakika zake pindi anapojiunga vifurushi vyao na amewataka kuacha mara moja tabia hiyo.

Hivyo ameomba serikali kuingilia kati suala hilo ili kuwasaidia wananchi ambao ni wahanga wa wizi huo unaofanywa na mitandao ya kijamii.

”Mitandao ya kijamii kudanganya wateja unanunua muda wa maongezi, unaandika dakika ulizotumia, kama ulikuwa na dakika 200 ukifikisha dakika 45 wanakwambia dakika zako karibu zinakwisha ukipiga tena wanakukatia wanakwambia dakika zako zimekwisha, wizi unatokea sana katika mitandao kwa bahati mbaya mimi kwa experience yangu simu yangu ya vodacom inaniibia sana muda wa maongezi, wakati umefika kwa serikali kuingilia mitandao hii ili isiendelee kuwaibia wananchi, na tumepata nafasi hii kuongea hapa watu wa vodacom wasikie  kuwa sio vizuri kutuibia pesa zetu tunazoweka huko” amesema Maghembe.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watu wanalalamika sana kuhusu wizi ulioko kwenye kampuni hizi za simu hasa kampuni za simu za Tigo na Vodacom, nikija kwenye tigo nao wanatuibia sana kila ukiweka salio wanakata kisha unatumiwa ujumbe kuwa bado unadaiwa mia tano sasa ili kuwakomesha na wizi wao nikitaka kununua muda wa maongezi nanunua moja kwa moja kwenye Mpesa ama Tigo pesa.

    ReplyDelete
  2. Makampuni ya simu yanayolalamikiwa yaitwe yaonywe ili yawache tabia hiyo na kama kuna wafanyakazi wasio waaminifu watimuliwe kazi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad