Mahakama Yawazuwia Viongozi wa Chadema Kusafiri Nje ya nchi

Hakimu mkazi wa mahakama ya Kisutu amekataa maombi ya kusafri nje ya maafisa wawili wa Chadema, limeripoti gazeti la The Citizen nchini humo.

Maafisa hao wawili wanaokabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo ni Katibu Mkuu wa Chama Dkt Vicent Mashinji na mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko.

Wawili hao, kupitia mawakili wao walikuwa wameomba mahakama iwaruhusu wasafiri nje ya nchi kushiriki mkutano.

Dkt Masinji, Bi Matiko na viongozi wengine wa ngazi ya juu wanakabiliwa na mashtaka ya uasi katika mahakama hiyo.

Jumanne Septemba 24, 2019 kupitia wakili wao Profesa Abdallah Safari waliiomba mahakama kuahirisha kesi dhidi yao ili kuwaruhusu wasafiri ng'ambo.

Dkt Safari aliiambia mahakama kwamba Dkt Masinji anatakiwa kusafiri kuelekea London Uingereza tarehe 26 septemba mwaka huu , ambako alitakiwa kuhudhuria mkutano tarehe 6 Oktoba.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Wafuasi wa Chadema
Kwa upande mwingine , Bi Matiko alitakiwa kusafiri kuelekea Kigali Rwanda Septemba 25 ana baadae kwenda mjini Brussels, Ubelgiji kuhudhuria mkutano kati ya tarehe 13 na 18 Oktoba mwaka huu.

Akitoa hukumu juu ombi hilo hakimu Thomas Simba, alisema kuwa kutokana na kwamba mahakama imebaini kuwa washtakiwa wanakesi ya kujibu ,kuwaruhusu kusafiri kutachelewesha mchakato wa kesi hiyo.

"Washtakiwa wanapaswa kuanza kujitetea juu ya mashtaka yanayowakabili, kwa hiyo kwa kuwaruhusu wasafiri itachelewesha kesi ," alisema Bwana Simba.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad