Mamia Wajitokeza Kuuaga Mwili wa Pacha

Mamia ya wakazi wa wilaya ya Missenyi mkoani Kagera wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Dennice Mwila wamejitokeza kuuaga mwili wa pacha Anisia Beatus aliyefariki dunia Septemba 3, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Siku chache baada ya kurejea kutoka nchini Saud Arabia, Anisia alifanyiwa upasuaji na mwenzake Merines Beatus baada ya kuzaliwa wakiwa wameungana.

Akizungumza wakati wa suala ya mazishi, Shehe wa Wilaya ya Missenyi, Abduzaidi Chagulani aliwataka Watanzania nchini kuwa na upendo wa dhati baina yao na kushikamana kwa pamoja wakati wa dhiki na raha. Alisema imekuwa ni mara chache watu kushikamana pamoja.

Alisisitiza kuwa vitabu vya dini vinataka amani, mshikamano na umoja. Aliwataka watu kuacha tabia ya kubaguana na kwamba hata vitabu vita- katifu vinapinga kubaguana.

Kwa upande wake, daktari bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Zaituni Bokhari aliyekuwa akiwahudumia pacha hao tangu walipowasili nchini wakitokea Saudi Arabia, alisema hali ya Anisia ilianza kubadilika akiwa safarini na kutapika mara kwa mara, hivyo kupoteza madini chumvi mwilini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad