Maombi ya msamaha kwa Washtakiwa uhujumu uchumi yaanza


Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Balozi Augustine Mahiga amesema washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi walio tayari kuomba msamaha na kusamehewa wameanza kufanya hivyo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

DPP, Biswalo Mganga ameanza kupokea maombi hayo kwa kasi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa pendekezo la Rais wa Tanzania, John Magufuli alilolitoa juzi baada ya kumaliza kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua.

Rais Magufuli alitoa siku saba kwa washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi walio tayari kuomba msamaha kufanya hivyo huku akiweka sharti kwamba wanaostahili msamaha ni wale watakaokuwa tayari kurudisha fedha walizotakatisha.

“Hapa tunavyozungumza nimetoka kuzungumza na DPP ananiambia maombi yanaingia kwa kasi sana na sasa lazima wafanye uchambuzi,” alisema Mahiga katika mahojiano na televisheni na Azam.

“Si suala tu la kutazama kesi moja, lazima kutazama mafaili, kutazama chimbuko lake kwa kushirikiana na idara ya upelelezi,” amesema Balozi Mahiga,.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad