Mavunde alia na wazazi wa Jimbo lake, awataka wasivione vyuo kama Mapambo

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Ajira, Kazi na Vijana, Antony Mavunde amewasisitiza wazazi kuhakikisha wanatumia fursa ya uwepo wa shule na vyuo vingi ndani ya jiji hilo kuwapeleka watoto wao kupata Elimu badala ya kuwaacha wageni peke yake.



Mavunde ameyasema hayo Septemba 27 mwaka huu  jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuwapongeza waalimu wa Shule ya Msingi Mlimwa B kwa kufaulisha vizuri wanafuzni katika matokeo ya bDarasa la saba.

Akizungumza katika hafla hiyo,amesema kuwa amekuwa akisikitishwa na baadhi ya watu katika mikoa mbalimbali hasa Dar es Salaam pindi wanapohitaji wafanyakazi wa ndani wanapiga simu Dodoma jambo linaloashiria kuwa na watu wengi wasio na elimu.

Kufuatia hilo pia amesema ni vyema wakazi wa Dodoma wakatumia fursa aliyoitoa Mh,Rais Dkt.John Magufuli ya Elimu bure kuwapeleka watoto wao kupata Elimu ili kujikomboa na Umasikini lakini pia vyuo mbalimbali vilivyopo wasivione kama mapambo.

"Huwa najisikia vibaya sana pale watu wa Dar es Salaam na Mikoa ya jirani pindi wanapohitaji wafanyakazi wa ndani simu ya kwanza wanapiga Dodoma,hili inabidi tulipinge,na tutalipinga kwa kuwasomesha watoto wetu"Alisema.

"Mkoa wa Dodoma unazidi kupiga hatua katika sekta ya Elimu,niwasihi wazazi tuzitumie shule na vyuo vya hapa kuwasomesha watoto wetu,tusivione vyuo vilivyopo kama mapambo maana kuna baadhi ya wazazi bado wana desturi ya kudharau Elimu"Aliongeza.

Aidha pia Mavunde ameahidi kuendelea kuborsha sekta ya Elimu katika jimbo lake kwa kutatua changamoto mbalimbali za miundombinu,upungufu wa madarasa,ofisi za walimu pamoja na vitendea kazi,ambapo ameahudi kupunguza tatizo la walimu wa sayansi katika Shule za Sekondari kwa kusambaza Kompyuta na kutumia mwalimu mmoja kufundisha shule zote kwa njia ya mtandao.

"Kiu yangu hasa katika Sekondari,najua kuna upungufu wa tatizo la walimu wa masomo ya Sayansi,sasa nataka kupunguza tatizo hilo,nataka nitoe Kompyuta kwenye Shule zangu zote na kisha kuunganisha mtandao ambapo Mwalimu mmoja atakuwa anafundisha Wanafunzi wa Shule zote kupitia mtandao,"Alisema.

Pamoja na kueleza baadhi ya changamoto ambazo bado zinawakabili, Mwalimu mkuu wa Shule hiyo Asha Maulid amempongeza Mbunge Mavunde kwa maendeleo makubwa aliyoyafanya katika Shule hiyo na kumuomba kuendelea kuifanya kwa maslahi mapana ya kukuza Elimu katika jimbo lake.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mheshimiwa hiyo approach ya kutumia computer ili Mwalimu mmoja afundishe wote! Mimi niaipinga kwa nguvu zote, kwani inaleta ufukara kwa taifa na ni adui mkuu wa kupunguza ajira kwa binadamu. Ningekuelewa vizuri endapo ungesema umeandaa Mpango maalum wa kuhamasisha watu ikiwemo kutoa motisha fulani kwa waalimu au wanafunzi Watakao somea sayansi ili waje kuwa waalimu wa somo hilo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad