Mbowe Ahoji Juu ya Kanuni Zitakazotumika Katika Uchaguzi ujao
0
September 05, 2019
Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amehoji juu ya kanuni zitakazoendesha uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, ambapo amesema kanuni hizo hazijapitiwa na Bunge.
Freeman Mbowe ametoa hoja hiyo Bungeni jijini Dodoma, wakati wa muendelezo wa vikao vya Bunge, ambapo amedai matumizi hayo ya kanuni ambayo inampa Mamlaka Waziri wa TAMISEMI kusimamia uchaguzi inaweza kuleta matatizo.
"Inawezekana tukaona mambo ya uchaguzi ni mepesi, lakini amani ya Taifa hili, inaweza kupotea kama tusipozingatia suala hili, sheria ndogondogo zinapotungwa lazima zipitiwe na Bunge, lakini Kamati ya Bunge haijawahi kuona au kupitia kanuni hizi za TAMISEMI". amesema Mbowe
Akijibu hoja hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dokta Adelardus Kilangi amesema, suala la kanuni kupitishwa na Bunge si lazima.
"Suala alilozungumza Mheshimiwa Mbowe kwa mujibu wa utaratibu sio sahihi, sheria zikishatayarishwa zinaletwa ofisini kwangu, kwa ajili ya uchambuzi halafu anazirudisha ili yeye azichapishe kwenye gazeti". amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Tags