Mbunge ataka sheria iundwe dhidi ya wanaotoa ushuzi ‘Kujamba’


Mbunge mmoja wa magharibi mwa Kenya amewasilisha pendekezo lake bungeni akitaka kuwekwa kwa sheria ya kudhibiti utoaji wa ushuzi katika safari za ndege.



Mbunge huyo wa jimbo la Rangwe Dkt Lilian Gogo alilitoa pendekezo hilo wakati wa kipindi cha hoja juu ya kufanyiwa kwa marekebisho ya sheria za usafiri ndege ili kuboresha usalama.

Dkt. Gogo aliliambia bunge kwamba utovu wa usalama hausababishwi tu na injini kufeli au mitambo mingine bali na wasafiri wanaotoa ushuzi safarini.

Alisisistiza kwamba wahudumu kwenye ndege wanapaswa kupewa mafunzo maalum ili kuwawezesha kudhibiti viwango vya ulevi wa abiria kwenye ndege akisema kwamba utovu wa nidhamu mara nyingi husababishwa na abiria waliobugia vileo.



“Kuna kitu kimoja ambacho hukera sana… na ni viwango vya utoaji wa hewa chafu. Kuna abiria ambao wanaweza kukera abiria wenzao kwa kutoa hewa chafu, inayonuka vibaya,na kukosesha starehe. Kama hili halitathibitiwa itasababisha ukosefu wa starehe ambayo itapelekea kuwepo kwa ukosefu wa usalama.” Alisema Dkt Gogo.

ushuzi
Mbunge huyo wa eneo bunge la Rungwe alisema kwamba mfumo maalum unapaswa kuwekwa ambao utathibiti vyakula vinavyopewa abiria kweny ndege na pia dawa zitakazosaidia kupunguza gesi.

“Kama kuna kitu ambacho hukera sana na husababisha watu kupigana ndani ya ndege ni utoaji wa ushuzi… Ni mbaya sana. Hata hapa nchini Kenya unaposafiri kutoka Kisumu hadi Nairobi au Nairobi kuelekea Mombasa…Mheshimiwa spika, kama ni mimi pekee ambaye nimekumbana na hili… Basi nadhani Bwana Spika, wengi wenu mna bahati sana…” Dkt Gogo alisema huku akionekana kukerwa.

” Kwa hivyo tunapaswa kuwa na dawa za kupunguza gesi ambazo zitatolewa kwa ndege… Na hili ninasema Bwana Spika linapaswa kufanyika , na linapaswa kuwa ni jambo ambalo linatambulika kisheria”

Dkt Rungwe alisisitiza kwamba wakati kuna abiria yeyote ambaye ana matatizo ya kiafya , usalama wa abiria wengine huathirika.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mie nnaufumbuzi wa hili tatizo..!!

    Isipo kuwa mwanzo nnataka kujua bei ya
    kilo moja ya Maharage ni kiasi gani.?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad