Mchungaji Mashimo Aeleza Alivyoacha Kazi TANROADS

 

Mchungaji Daud Mashimo amesema kuwa kabla ya kuwa mchungaji aliwahi kufanyakazi katika ofisi ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kama mkaguzi wa hifadhi za barabara lakini masuala ya kiutendaji ndiyo yalimfanya aache kazi hiyo.


Mchungaji Mashimo ameyabainisha hayo wakati akielezea masikitiko yake baada ya TANROADS kuzichukua spika anazotumia kufanyia mahubiri  kwa mara ya pili sasa.

Sababu ya kunyang'anywa spika hizo ni madai ya kwamba amekuwa akisababisha kelele na bugudha kwa watu ilihali anavyo vibali vya kufanya mahubiri hayo kutoka Wizara ya Mambo ya ndani na kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi.

''Mimi nilikuwa mtumishi  wa TANROADS na nimetumikia kwa muda wa miaka mitano, mimi nimempokea Kristu muda mrefu na mimi kazi yangu ilikuwa nikutoa notisi ya kubomoa majengo yaliyokuwa ndani ya hifadhi ya barabara'', amesema Mashimo.

Kwa upande wa TANROADS kupitia kwa meneja wake, Eng. Ngusa amesema kuwa hawezi kutoa maelezo yoyote kuhusu suala la mchungaji Mashimo na kwamba kama anahitaji ufafanuzi aende katika ofisi hizo.

Spika anazozilalamikia Mchungaji Mashimo zilikimatwa Septemba 3, 2019, alipokuwa akifanya mahubiri kwa wasafiri katika stendi ya mabasi ya Mbezi Jijini Dar es Salaam na yeye ameshindwa kuchukua hatua zozote na badala yake anamuachia Mungu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad