Mfahamu Mzee Aliyetembea Kwa Miguu Kilwa Mpaka Dar es Salaam
0
September 27, 2019
Watanzania wametakiwa kuenzi fikra za muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo, ili kufikia misingi ya umoja na mshikamano katika Taifa.
Akizungumza leo Septemba 25, 2019 Mzee Ally Issa Gereku, aliyewahi kutembea kwa mguu kutoka Kilwa hadi Dar es Salaam kwa siku saba, ili ya kuunga mkono Azimio la Arusha, wakati wa mhadhara wa sita wa Kavazi cha Mwalimu Nyerere, amesema enzi zao walikuwa wakifanya shughuli kwa kujipatia chakula na si biashara.
"Sisi watoto tulijilea wenyewe na wazazi wetu walikuwa wanalima chakula tu hakuna zao la biashara, kwa hiyo hata ukilima ukavuna kwa kiasi gani, unavuna chakula lakini si kwa biashara" amesema Mzee Ally.
Mzee Ally Gereku anadai kuwa yeye alizaliwa mwaka 1952, katika familia masikini na kutokana na mafunzo waliyoyapata shuleni ndiyo yaliyompa nguvu na moyo wa kutembea.
Tags