Mke Aua Mumewe Mzungu na Kumtupa Kwenye Shimo la Choo


Sarah Wairimu Kamotho ambaye ni mke wa tajiri aliyeuawa Tob Cohen awasili kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Chiromo kuhudhuria upasuaji na uchunguzi wa maiti ya mumewe, baada ya wakili wake kumtaka awepo ili ashuhudie. Upasuaji huo uliahirishwa jana ili Sarah Wairimu aweze kuhudhuria.

Tajiri mkubwa huyo wa Kidutch Tob Cohen aliyekuwa anaishi na mke wake raia wa Kikenya (Mkikuyu) hatimae mwili wake ulikutwa kwenye septic tank ukiwa umeharibika vibaya, huku akiwa amevunjwa mkono na viungo vingine.

Ndoa yao ilikuwa na misukosuko hasa kwa kile kinachoelezwa mwanadada Sarah Wairimu hakuwahi kumpenda yule baba wa miaka 72 isipokuwa alipenda pesa tu.

Tob Cohen hakuficha marafiki zake kwa namna alivyokuwa anateswa na mke wake ambaye alimpenda kwa dhati.

Kuna kipindi alimtumia dada yake video akivuja damu baada ya kupewa kipigo na huyo slay queen wa Kikenya.

Rafiki yake wa karibu anadai ni mara nyingi Cohen alikuwa anamwambia nahofia ipo siku mkewe anaweza kumuua na akifa wala wasisumbuke kutafuta mchawi.

Tob Cohen alipotea katika mazingira ya kutatanisha huku mkewe mshenzi yule akiwaambia rafiki zake mmewe kuwa alisafiri kwenda Thailand kutibiwa!!

Marafiki na ndugu walipeleka taarifa ya wasiwasi wao kwa ubalozi wa Dutch hapo Nairobi na juhudi za kumtafuta zikapamba moto.

Baadae walinzi walihojiwa endapo ni kweli boss wao alisafiri wakasema ni kweli.

Wakaulizwa aliondoka nyumbani kwa mguu au gari wakasema aliondoka na gari kwenda airport!! Wakaulizwa dreva aliyekuwa anaendesha gari ni nani wakakosa jibu.

Maafisa wakaenda airport kutafuta ukweli wa safari yake pale airport hakukuwa na jina la Cohen akitoka nje ya nchi!

Wakaenda kwenye mipaka ya Kenya ya njia za ardhi nako hakuna kitu!!. Mwishowe wakamkamata yule mkewe na kwa jeuri katika kesi hiyo mke akatafuta mwanasheria maarufu Kenya kwa ajili ya kujitetea kuondokana na tuhuma hizo, akiwa bado mahabusu mpepelezi mkuu Kenya na vijana wake Wanaendelea na uchuguzi ndipo wakaona "Karo" ambalo linatunza uchafu likiwa mfuniko wake umesilibiwa na simenti mpya kabisa na walipolifungua tu wakamkuta tajiri huyo akiwa amefungwa kwenye mfuko wa nailoni akielea kwenye maji taka hapo hapo nyumbani kwake ndani ya uzio!!.

Inasemekana aliyewaambia mwili ulipo ni rafiki yake wa kike wa mke wa marehemu ambaye na yeye amekamatwa na kupewa suruba na wazee wa kazi ndipo akawaambia A-Z kuwa marehemu aliuliwa ndani ya nyumba hiyo na kuzikwa hapo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad