Mkuu wa Wilaya Aagiza Tanesco Kukatiwa Umeme Katika Ofisi yake
0
September 25, 2019
Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai, Ole Sabaya ameliagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Wilayani humo, kukata mara moja umeme katika Ofisi za Halmashauri ya wilaya hiyo baada ya halmashauri hiyo kushindwa kulipa bili ya Soko Kuu la Hai kwa muda wa miezi miwili.
Akizungumza na EATV & EA Radio Digital leo Septemba 25, 2019 Sabaya amesema kuwa ameagiza iwe hivyo kwa sababu hawezi kuvumilia kuona wananchi wanaolipa kodi wanaendelea kunyanyasika na kufanya shughuli zao kwenye mazingira magumu na hivyo anaona ni vyema wao wapate umeme na halmashauri ikose.
'' Soko Kuu la Hai halina umeme kwa muda wa miezi miwili, kisa tu halmashauri ambayo inatoza ushuru hapo haijalipa deni , mimi sipo tayari kufanya kazi katika ofisi isiyo na umeme na sipo tayari kuona wananchi wanatozwa kodi na hairudi kulipa deni la umeme'', amesema Sabaya.
Sabaya ameagiza hatua za kukatwa umeme katika ofisi hiyo zifanyike siku ya leo.
Tags