Mkufunzi wa zamani wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho anaamini kwamba mchezaji wa miaka mingi Sameul Eto’o alistahili kutwaa tuzo Ballon d’Or walau moja.
Samuel Eto'o and Jose Mourinho embrace after Inter Milan won the 2010 European Champions League
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona mwenye umri wa miaka 38 alistaafu hivi karibuni katika mchezo wa soka.
Moja kati ya matokeo yake bora kabisa kwenye kipindi chake cha miaka 22 ambao ulihusisha kushinda kombe la bara Afrka mara mbili na kombe la mabingwa Ulaya mara tatu.
Mourinho kwa mara ya kwanza alifanya kazi na mchezaji huyo akiwa Inter Milan wakati wa msimu wa 2009/2010 ambapo wawili hao walishinda mataji matatu katika msimu mmoja likiwemo taji la Serie A, Kombe la Itali na kombe la mabingwa Ulaya.
Image result for Mourinho vs Samuel Eto'o Inter Milan
Wawili hao kwa mara nyengine walifanya kazi pamoja katika klabu ya Chelsea miaka mitatu baadaye kwa muda mfupi.
”Ni vigumu kuelewa ni kwa nini Eto’o hakushinda taji la Ballon d’Or kufuatia kipindi chake cha soka” , alisema Mourinho katika mahojiano na Radio Cameroon.
”Samuel alichezea timu bora katika ligi bora duniani. Alifunga magoli mengi mazuri na alifanikiwa akiwa katika ligi tofauti”, aliongezea.
Alishiriki katika fainali tatu za ligi ya mabingwa Ulaya , akishinda mara mbili na Barcelona huku akifunga katika fainali zote mbili.
Pia alishinda kombe la mabingwa Ulaya mara moja akiichezea Inter mbali na kushinda mataji mengi ya ligi.
”Alikuwa mshambuliaji bora duniani kwa miaka kadhaa na nafikiria alihitaji kushinda taji la Ballon d’Or lakini haya ni mambo ambayo hatuna udhibiti nayo”.
Samuel Etoo alishinda mara nne taji la mchezaji bora wa Afrika huku tuzo bora ya fifa aliyopata ni ile ya kuwa katika nafasi ya tatu 2005.
Mbali na kushinda kombe la mataifa ya Afrika 2000 na 2002 aliibuka kama mfungaji magoli mengi akiwa na magoli 18.
Eto’o ni mchezaji wa kipekeeCameroon's Samuel Eto'o aliibuka wa tatu katia tuzo za Fifa 2005 nyuma ya kiungo wa kati wa Frank Lampard na mshindi Ronaldinho wa BrazilCameroon’s Samuel Eto’o aliibuka wa tatu katia tuzo za Fifa 2005 nyuma ya kiungo wa kati wa Frank Lampard na mshindi Ronaldinho wa Brazil
Mchezaji huyo wa zamani wa Everton na Chelsea ni miongoni mwa wachezaji wa Afrika akiwemo Didier Drogba , Michael Essien na John Obi Mike ambao walitia fora chini ya ukufunzi wa Jose Mourinho lakini ‘The Special One’ anaamini kwamba nahodha huyo wa zamani wa Cameroon alikuwa mchezaji tofauti.
Kipindi cha mchezo wa Samuel Eto’o kilikuwa kizuri sana na kitu muhimu kwa mchezaji ni mchango wake katika timu yake kupata ushindi.
Alikuwa akitumia kila njia timu yake kuweza kupata ushindi. Samuel alikuwa mchezaji aliyekuwa na kipaji lakini alishirikiana sana na wenzake. Alishinda mataji yote muhimu na akapata ufanisi mkubwa katika kipindi chake cha mchezo.
”Akiichezea Inter tulicheza dhidi ya Barcelona katika nusu fainali ya ligi ya mabingwa , tulikuwa na wachezaji 10 na Eto’o alicheza mechi yote. Alijitolea na kucheza katika safu hiyo ili kuhakikisha kuwa tunapata ushindi. Hicho ndio ambacho timu ilihitaji wakati huo”.
”Mjini Milan tulikuwa tumeshinda magoli 3-1, tulipokuwa tukielekea Camp Nou, hatukuhitaji kufunga, tulihitaji kutinga fainali na alielewa hilo”.
Alifanya kila kilichohitajika kwa timu kufuzu fainali. Hii ni tabia nzuri katika binadamu na nina hakika Eto’o atafanikiwa baada ya kustaafu”.
Samuel Eto’o alichezea klabu 13 katika mataifa sita na kufunga jumla ya magoli 56 katika mechi 118 akiichezea Cameroon.