Mshtakiwa amuandikia barua DPP kuomba kukiri kosa la kusafirisha madini
0
September 28, 2019
Raia wa Sri Lanka AbdulAzeez Amaan (26) amemuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuomba kukiri kosa la kusafirisha madini yenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 36 kinyume cha sheria.
Amaan ambaye ni mwanafunzi amefikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha madini hayo bila ya kuwa na kibali cha Kamishna wa Madini nchini.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alimsomea mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Wankyo alidai kuwa Septemba 21 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere uliyopo Ilala Jiji Dar es Salaam mshtakiwa huyo alikutwa akisafirisha madini aina ya Scapolite yenye uzito wa gramu 996.50, Sperssartite gramu 487, Tanzanite gramu 44, Quarts gramu 126, Citrine gramu 174, blue agate gramu 101.80, Toumarine gramu 16, Aquamarine gramu 14.30 na Supphire gramu 5.04 yote kwa pamoja yakiwa na jumla ya Sh. Milioni 36.5 bila ya kuwa na kibal
Tags